ENGLISH
Serve Salama is Tanzania’s first dedicated responsible alcohol service and sales online training program, it is created to promote safe, legal, and ethical alcohol practices across the country.
Modelled after global best practices and tailored to Tanzania’s laws, cultural values, and community needs, Serve Salama empowers alcohol servers, sellers, and delivery staff with the knowledge and tools they'd need to:
Prevent underage access to alcohol
Recognize signs of intoxication
Make informed, legal, and safe service decisions
Support a healthier, more responsible hospitality and retail industry
By equipping everyone involved in the alcohol service and sales with the essential skills, Serve Salama champions community public safety first, accountability, responsibility, and general public well-being.
SWAHILI
Serve Salama ni programu ya kwanza ya kidigitali hapa nchini Tanzania inayojikita katika mafunzo ya huduma na uuzaji wa pombe kwa uwajibikaji, mafunzo haya yameundwa kwa ajili ya kukuza na kudumisha mazoea salama, kisheria, na ya kimaadili ya pombe kote nchini.
Imeundwa kwa kuzingatia mifumo bora ya kimataifa na kurekebishwa kulingana na sheria, tamaduni, na mahitaji ya jamii ya Tanzania, Serve Salama inawapa wahudumu wote wa pombe, wauzaji, na wafanyakazi wa usafirishaji wa pombe maarifa na zana muhimu za:
Kuzuia mauzo ya pombe kwa waliochini ya umri wa kisheria
Kutambua ishara za ulevi wa kupindukia
Kufanya maamuzi sahihi, kisheria, na salama katika huduma
Kusaidia sekta ya ukarimu na maduka kuwa na afya na uwajibikaji zaidi
Kwa kuwapatia wahusika wote katika utoaji wa huduma ya pombe uwezo muhimu, Serve Salama inakuza usalama wa jamii, uwajibikaji, majukumu binafsi, na ustawi wa umma.